Israel inajiandaa kwa maandamano mjini Jerusalem baadaye leo, huku kukiwa na hofu ya kutokea tena machafuko mjini humo ambapo jeshi la Israel limetuma vikosi vya ziada Ukingo wa Magharibi ambako kuna uwezekano wa machafuko kuenea hadi eneo hilo.

Kwa mujibu wa gazeti la Jerusalem Post,Waisraeli takriban 5,000 wenye misimamo mikali ya kizalendo wanatarajiwa kuandamana wakiwa wamebeba bendera za taifa katika eneo la mji mkongwe.

Maandamano hayo yameandaliwa na wafuasi wa waziri mkuu wa zamani, Benjamin Netanyahu, ambaye anaendelea kuishinikiza serikali ya waziri mkuu mpya Naftali Benett.

Wapalestina wanayaona maandamano hayo kama uchokozi na makundi ya Fatah na Hamas yameitisha siku ya ghadhabu na kisasi.

Hayati TB Joshua kuzikwa kanisani
Wasanii kuanza kulipwa kuanzia Disemba