Mashairi yaliyoandikwa kwa mkono ya Tupac Shakuru akiwa gerezani ya ‘Ambitionz As A Ridah’ yaliyoandikwa kwenye karatasi mbili tofauti yatapigwa mnada na kumilikishwa kwa mtu yoyote.

Kwa mujibu wa ITV ya Marekani, mashairi hayo aliyoyaandika akiwa jela mwaka 1995 yatapigwa mnada mwishoni mwa mwezi huu jijini London, Uingereza. Yanatarajiwa kuuzwa kati ya $47,000 na $78,000.

‘Ambitionz Az A Ridah’ ilitumika kama utangulizi wa album ya nne ya Tupac ‘All Eyez on Me’ iliyokuwa album ya mwisho kabla hajauawa kwa risasi mwaka 1996. Album hiyo iliwashirikisha wakali kama Snoop Dogg na Dr Dre.

Aunt Ezekiel Aihama Ukawa? Mwenendo Wake Unaongea
Polisi Wasusia Posho Baada Ya Kazi