Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amevunja Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini – REA, na kumteua Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Gideon Kingu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini – REA.
Aidha, Rais Samia pia amerudisha Mhandisi Peter Ulanga kuendelea kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, nafasi ambayo alikuwa amepewa Maharage Chande ambaye naye sasa ameteuliwa kuwa Postamasta Mkuu.

Kabla ya mabadiliko haya, Mhandisi Ulanga alitolewa katika nafasi hiyo huku Chande akiteuliwa katika nafasi hiyo aliyohudumu kwa siku tatu kuanzia Septemba 23-25, 2023, akitokea kwenye nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini – TANESCO.