Kupitia utafiti wao, Wanasayansi Barani Ulaya wamebainisha kuwa mabadiliko ya hali ya hewa ndio chanzo kikuu cha mafuriko yaliyoua zaidi ya watu 600 nchini Nigeria mwaka huu wa 2022.
Katika utafiti huo, wanasayansi hao wamedai kuwa mafuriko yaliyoathiri nchi za Nigeria, Niger, Chad, na nchi nyingine za jirani yalihusishwa moja kwa moja na shughuli za binadamu.
Kwa mujibu wa wataalamu hao, mafuriko hayo ya kati ya Juni na Oktoba 2022 yalisababisha zaidi ya watu milioni 1.4 kuyahama makazi yao na yalikuwa na uwezekano wa kutokea mara 80 kutokana na shughuli za kibinadamu.
Ripoti hiyo inakuja wakati yamefanyika mazungumzo ya COP27 ya hali ya hewa yakiendelea huko Sharm el-Sheikh nchini Misri, ambapo mataifa yanayoendelea yanadai wachafuzi wa mazingira matajiri walipe majanga yanayohusiana na mabadiliko ya tabianchi.