Serikali inatarajia kunufaika na takribani shilingi trilioni 2.44 kwa mwaka kutokana na Biashara ya Kaboni, ambapo mapato hayo yanatarajia kukuza uchumi wa nchi na kusaidia kupambana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi ambayo ni changamoto ya dunia, na muhimu kuendelea kutoa elimu ya kukabiliana nazo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dkt. Selemani Jafo wakati akifungua Majadiliano ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kuhusu Biashara ya Kaboni kilichofanyika jijini Dar es Salaam, kupitia Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dkt. Selemani Jafo.

Amesema, “ni matarajio yetu kuwa Biashara ya Kaboni itasaidia kupunguza kiwango cha gesijoto kwa asilimia 30 hado 35 ifikapo mwaka 2023 hivyo tutaendelea kuongeza nguvu katika kushirikiana na wadau katika kufanikisha hatua hii.”

Kwa upande wake, Kaimu Mtendaji Mkuu wa TPSF Raphael Maganga ameishukuru Serikali kwa jitihada zake za kukabilianja na athari za mabadiliko ya tabianchi na katika nyanja mbalimbali hapa nchinina kwamba mabadiliko ya tabianchi ni changamoto ya dunia hivyo ni muhimu kuendelea kutoa elimu ya kukabiliana nazo.

Mtu mmoja hawezi kuwapotosha werevu watatu - Mjengwa
Malumbano hayawezi kupewa nafasi - Rais Dkt. Samia