Kutokana na teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA), kuwa na mabadiliko ya mara kwa mara umuhimu wa kuandaliwa kwa mafunzo ya usalama wa mitandao unahitajika nchini.
Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma na mwakilishi wa Wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Richard Mgema wakati akifunga shindano la wanafunzi wa vyuo vikuu nchini lililoandaliwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), lililohusu usalama wa mitandao.
Amesema Dunia imekuwa katika mabadiliko ya tehama kila iitwapo leo na kwamba Tanzania haiwezi kuwa kisiwa cha kutoendana na teknolojia hivyo inayohitaji mafunzo ya usalama wa kimitandao.
Serikali yaongeza mbinu ufaulu somo la Sayansi na Hisabati
“Kama nchi kumekuwa na mabadiliko ya huduma za fedha kwenda katika mitandao hivyo vijana wengi wanahitajika kuhusiana na kujua mifumo ya ulinzi wa mitandao ili Fedha za Wananchi ziwe salama,” amebainisha Mhandisi Mgema.
Aidha ameongeza kuwa ukuaji wa tehama ni wa kasi kutokana na mifumo ya kiteknolojia kubuniwa hivyo lazima kuwapo kwa rasilimali watu ya kuendana na wakati husika katika Teknolojia hizo.
mlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kanda ya kati Antonio Manyanda amesema usajili wa shindano la usalama wa mitandao ulikua na wanafunzi 1,056 na baada ya mchujo wa kwanza walibaki 600 na mchujo wa tatu walipatikana wanafunzi 50 kutoka vyuo vikuu nane nchini.
Amesema wanafunzi hao waliokuwa na wanaoshiriki shindano hilo ni wale wanaosoma teknolojia ya Habari na mawasiliano yaani (IT) na umri wao ni kati ya miaka 18 hadi 24.
“Walioshiriki wote ni washindi maana wamepita katika makundi mbalimbali hata kwenye mchujo hadi kufika hatua ya mwisho ya kupatikana kwa washindi wawili,” amefafanua Manyanda.
Naye Mkurugenzi wa Tehama wa (TCRA), Connie Francis amesema kuwa katika shindano hilo amegundua kundi la wasichana halipo nyuma kwani wameonesha ukomavu wao kwa kujitokeza kushiriki shindano hilo na kuwataka washiriki wote kuendelea kusoma kwa bidii ili kuleta mabadiliko ya Tehama.
Washindi wa Shindano hilo lililoandaliwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), kwa kushirikiana na kampuni moja ya nchini Kenya ni Godwin Mpapalika ambaye ni mshindi wa kwanza na Karim Muya aliyeshika nafasi ya pili.