Kamati ya Utendaji ya Young Africans imepokea na kuridhia rasimu za Mabadiliko ya Muundo wa Uendeshaji wa Klabu kutoka katika Kamati ya mabadiliko Katiba na kuruhusu mchakato kuendelea kwa hatua inayofuata.

Kikao cha Kamati ya Utendaji kilichokutana Makao Makuu ya Klabu Jangwani, chini ya Mwenyekiti wa Dkt. Mshindo Msolla, kilipokea rasimu hiyo baada ya mchanganuo mkubwa uliofanywa kutoka kwenye mapendekezo ya La Liga na Kamati Mabadiliko.

Kaimu Katibu Mkuu, Haji Mfikirwa amesema baada ya kupokea rasimu hiyo Kamati ya Utendaji ambayo ndio chombo cha juu cha maamuzi kwenye Utendaji wa Klabu imeridhia mchakato huo kwenda katika hatua ya kushirikisha wadau ambao ni hatua ya mwisho.

“Sasa tunakwenda katika hatua ya mwisho ambayo ni kuwashirikisha wadau kwa maana ya vyombo vya Serikali, kama BMT, FCC, Wizara na Wadau wa soka, kisha tutarudi kwa Wanachama na mwisho kabisa katika Mkutano Mkuu ambao ndio ngazi ya mwisho ya kutoa maamuzi kwa klabu yetu kwa mujibu wa Katiba yetu ya sasa,” amesema Mfikirwa

Amesema kwa sasa Kamati ya Mabadiliko ya Katiba itamalizia mapendekezo kadhaa ya Kamati ya Utendaji kisha kuanzia wiki ijayo mchakato usonge mbele.

“Kwenye muundo kuna mabadiliko kadhaa ambayo yamepitishwa, hivyo Kamati ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Wakili Raymond Wawa itakaa mapema wiki ijayo kuyaakisi mabadiliko hayo kwenye Katiba pendekezwa kisha tunatakwenda kuwashirikisha wadau wa Serikali,” amesema muwakilishi mmoja.

Lee Clark aichimba mkwara Simba SC
Wafungwa wapigwa 'stop' kazi binafsi