Mwanamume mmoja ameshitakiwa baada ya kamera kadhaa za siri kupatikana katika vyumba vya wanawake vya kuoga katika ubalozi wa Australia jijini Bangkok nchini Thailand.

Wizara ya Masuala ya Nje na Biashara ya Australia imethibitisha kuwa polisi nchini Thailand walikamata mfanyakazi huyo wa zamani mwezi jana na msemaji wa wiazara hiyo alisema kuwa maslahi ya wafanyakazi wake ni suala la kipaumbele japo alikataa kuzungumza zaidi kuhusu mpango wa kisheria unaoendelea kuhusu tukio hilo.

“Maslahi na ufaragha wa wafanyakazi wote ni kipaumbele kwa Wizara hii na tutaendelea kutoa ushirikiano unaohitajika,” msemaji huyo alisema katika taarifa iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP.

Kamanda wa polisi wa Thailand wa masuala ya kigeni, Khemmarin Hassiri, alisema kuwa ubalozi wa Australia ulikuwa umetoa ripoti dhidi ya mwanamume mmoja mnano Januari 6 na kwamba uchunguzi ulikuwa unaendelea.

Haijulikani kamera hizo zimekuwa katika vyumba hivyo kwa muda gani na nia ya kuweka kamera hizo ni ipi, lakini suala hilo lilitokea kujulikana baada ya kadi ya kamera kupatikana katika sakafu ya vyumba hivyo.

Mtaalamu wa ulinzi na masuala ya kigeni ya Australia aliliambai shirika la habari la AFP kuwa tukio hilo lilidhihirisha ukiukaji wa taratibu za usalama.

“Kama usalama ulikuwa umepungua kiasi cha kuruhusu vifaa kama vile kamera kuweka mahali popote, inamaamisha kuwa ulinzi hata hautoshi kuuhakikishia ubalozi huo usalama wake,” alisema Hugh White, Profesa wa zamani katika Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Australia.

Wananchi walala juu ya miti licha ya kuwa na anyumba
Mtoto aliyenasa kwenye kisima afariki dunia