Bahran imeungana na Saudi Arabia kuvunja ubalozi na Iran kutokana na uvamizi wa ubalozi wa Saudi Arabia nchini Iran uliofanywa na watu wanaopinga hukumu ya mauaji ya mhubiri mashuhuri wa Ki-Shia, Sheikh Nimr al -Nimr na wenzake 46.

Bahran ambaye hutawaliwa na Mfalme Msuni huku ikiwa na raia wengi wa madhehebu ya Shia, imetoa saa 48 kwa mabalozi wote wa Iran kuondoka nchini kwake.

Uamuzi huo pia umechukuliwa na nchi ya Sudan ambaye imewafukuza mabalozi wote wa Iran kutoka Khartoum huku Muungano Jumuiya ya Miliki za Kiarabu (UAE) ikipunguza idadi ya maafisa wa ubalozi wa Iran.

Mbubiri wa Kishia, Sheikh Nimr al-Nimr aiuawa nchini Saudi Arabia na wenzake 46 baada ya kukutwa na hatia katika tuhuma za ugaidi zilizokuwa zinawakabiri.

Kufuatia hukumu hiyo, wananchi walifanya maandamano makubwa kupinga hatua hiyo huku wengi wao wakiwa waumini wa madhehebu ya Ki-Shia.

Saudi Arabia imeendelea kusisitiza kuwa hukumu yake dhidi ya mhubiri huyo wa Ki-Shia na wenzake ilifuata haki na ni sehemu ya juhudi za kutokomeza ugaidi. Serikali ya Iran imepinga vikali uamuzi huo wa Saudi Arabia na kueleza kuwa nchi hiyo itaujutia.

Mugabe, Museven Watahadharishwa kufungwa jela na Mgombea Urais Wa Marekani
Wanafunzi wa shule ya msingi wasomea chini ya Mti