Mabalozi kutoka nchi za ulaya, waliotembelea miradi inayotekelezwa na FETA ukiwemo wa utoaji elimu ya ufugaji samaki kwa njia ya vizimba kwenye Ziwa Victoria, wamesema wameridhishwa na namna fedha walizowekeza jinsi zinavyotumika na kuhamasisha vijana kuiomba serikali iwasimamie, ili waweze kutumia kwa malengo tarajiwa.

Mabalozi hao, walikuwa wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Mwanza mara baada ya kutembelea miradi hiyo na wamewaasa vijana kuchangamkia fursa hiyo kwa kuanza na kidogo walichonacho, ili waweze kufikia malengo yao waliyojiwekea maishani.

Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Prof. Mohammed Sheikh (wa kwanza kulia), akizungumza na mmoja wa mabalozi kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya waliotembelea Kampasi ya Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) iliyopo Kata ya Nyegezi jijini Mwanza, kushuhudia majukumu mbalimbali ya FETA na mradi wa ufugaji samaki wanaoufadhili. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa FETA Dkt. Semvua Mzighani.

Umoja wa Nchi za Ulaya umewekeza Shilingi Milioni 800 kwa Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi Tanzania (FETA), kwa ajili ya kukuza Sekta ya Uvuvi kupitia ufugaji samaki ambapo wanawekeza kwenye miundombinu.

Mwingine ni katika mitaala na kuwawezesha wakufunzi kupata elimu zaidi kwenye ukuzaji viumbemaji kwa njia ya kisasa katika kipindi cha miaka minne ambapo hadi sasa mradi huo umetekelezwa kwa miaka miwili ili kuvutia tasnia ya ufugaji samaki.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 29, 2023
Rais Samia azungumza na Mkurugenzi Kampuni ya mafuta UAE