Uongozi wa Mradi Wa Mabasi Yaendayo Kasi (Dart) umepiga marufuku uwekaji wa mabango na picha za wagombea wa nafasi za uongozi wa kisiasa katika vituo  vya mabasi jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Usafiri ‘Dart’, Mhandisi Serapion Tegawa alisema kuwa kitendo hicho hakikubaliki kwa kuwa ni kinyume cha taratibu na kwamba kinapelekea uchafuzi wa vituo hivyo.

Aliongeza kuwa kama wahusika wanatafuta sehemu za kuweka mabango ya wagombea wao wanapaswa kuwasiliana na manispaa ya jiji ili waelekezwe sehemu inayostahili.

“Ni vizuri wahusika wakafika katika Manispaa ili waelekezwe sehemu ya kuweka picha hizo kwa sababu matangazo na picha hizo huchafua vituo vyetu,” alisema na kuongeza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaoendelea kufanya vitendo hivyo.

Mbatia Ajibu Ya Dk. Slaa, Adai Sitta Na Mwakyembe Sio Saizi Ya Lowassa
Rivaldinho Wa Rivaldo Asajiliwa Boavista