Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene ameyaonya mabasi 16 ya abiria yanayofanya safari zake katika mikoa mbalimbali nchini kuacha mara moja tabia ya kuvunja Sheria za Usalama Barabarani zinazohatarisha maisha ya Watanzania wanaotumia huduma hizo za usafiri.

Simbachawene, ametoa onyo hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma alipokuwa akitoa taarifa kuhusu hali ya usalama na matukio ya ajali za barabarani nchini hususan katika kipindi hiki cha kuelekea Sikukuu za Krismas na Mwaka Mpya.

Mabasi yaliyoonywa ni pamoja na T367 ARH-Asante Rabbi yanayofanya safari zake za Arusha kuelekea Mwanza, T498 BYZ-Kidia One linalotoka Mwanza kuelekea Dar es Salaam, T395 BAP-Asante Rabbi linalotoka Arusha kuelekea Mwanza, T718 DPK-Maning Nice linalotoka Morogoro kuelekea Masasi, T695 DMJ-Ally’s Star linalotoka Dar es Salaam kuelekea Mwanza, T424 AWB-Mgamba linalotoka Mwanza kuelekea Arusha, T253 DHM-Capricon linalotoka Arusha kuelekea Mbeya, T400 AKM-Yellow line linalotoka Singida kuelekea Mbeya.

Mabasi mengine ni, T756 DNT-Ally’s Star linalotoka Mwanza kuelekea Dar es Salaam, T260 DUC-Frester linalotoka Dar es salaam kuelekea Mwanza, T221 DKB-Saratoga linalotoka Dar es Salaam kuelekea Kigoma, T988 AHB-Capricon, T450 AWJ-Frester, T774 DRL-BM linalotoka Arusha kuelekea Dar es Salaam, T768 DRL-BM linalotoka Arusha kuelekea Dar es Salaam, T775 DRL-BM linalotoka Arusha kuelekea Dar es Salaam.

Simbachawene, amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mabasi yote yanayokiuka Sheria za Usalama Barabarani, “Nimesema nitachukua hatua kali za kisheria kwa ajili ya mabasi yote niliyoyataja na yote yatakayobainika kuvunja Sheria zote za Usalama Barabarani, na hili nalisema kwa uwazi kabisa madereva acheni kuhatarisha maisha ya Watanzania” alisema Simbachawene.

Wachezaji FC Platnum wazuiwa kutumia simu
Sudan yakubali kuwalipa waathiriwa wa mashambulio ya Al-Qaeda