Serikali imeanza hatua za kufanya manunuzi ya mabasi 165 mapya ya mwendo kasi ili kuendelea kupambana na tatizo la foleni jijini Dar es Salaam na kuwarahisishia wakazi wa jiji hilo huduma za usafiri.

Akitoa maelezo ya huduma ya usafiri wa mwendo kasi mbele ya Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa jana, Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (DART), Ronald Rwakatare amesema kuwa mabasi hayo mapya yataanza kazi Aprili mwakani.

Alisema kuwa tayari mchakato wa manunuzi umeanza na uko kwenye hatua ya kumpata mzabuni ambaye atasaini mkataba Disemba mwaka huu.

“Haya mabasi yatahudumia maeneo ya Morocco, Masaki Tegeta, Makumbusho na baadhi ya maeneo mengine ambayo hayajafikiwa na mradi huu,” alisema Rwakatare.

Alieleza kuwa ujenzi wa miundombinu wa awamu ya pili ya mradi huo umeanza.

 

Dar: Kizimbani kwa kukutwa na ‘mihuri ya Ikulu, Mahakama Kuu’
Waziri aagiza Machinga waondolewe Kariakoo, ‘asema Rais hakumaanisha warudi’