Hatimaye wakazi wa jiji la Dar es Salaama leo wataanza kunufaika na huduma ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi (BRT) ulioanza kutayarishwa takribani miezi ishirini iliyopita.

Mabasi hayo yanatarajia kuanza kazi leo majira ya saa tatu kamili asubuhi yakianzia stendi ya mabasi yaendayo mikoni (Ubungo). Wakazi wa jiji hilo wataipata huduma hiyo bure kama sehemu ya kusherehekea uzinduzi.

Kwa mujibu wa Afisa anaeshughulika na masuala ya fidia katika mradi huo, Deusi Mutasingwa, mradi huo utaanza na mabasi ya aina mbili. Aina ya kwanza ni mabasi yenye uwezo wa kubeba abiria 140 na aina ya pili ni yale yatakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 80.

Uzinduzi wa mabasi hayo unafanyika ikiwa ni kipindi cha kwanza cha mpito huku Dar es Salaama ikiweka historia ya kuwa jiji la kwanza Afrika Mashariki kuanza kutumia mabasi hayo.

Mradi wa BRT ni sehemu ya juhudi za serikali kupunguza msongamano wa magari na kuwaondolea wakazi wa Dar es Salaam shida ya usafiri.

Joseph Butiku Apasua Jipu, "Nyerere Alipenda CCM Imeguke"
Pardew Aitambia Arsenal Kwa Cabaye