Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi, amefanya mazungumzo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Venance Mabeyo, ikulu ya Zanzibar, aliyefika kumuaga kufuatia kubaki siku chache ili  kumaliza muda wake wa utumishi.

Katika mazungumzo yao Rais Mwinyi amempongeza Jenerali Mabeyo kwa kutekeleza vema majukumu katika kipindi chake chote alichohudumu kama mtumishi ndani ya Jeshi hilo.

Aidha, Dkt. Mwinyi amemtakia kila la heri Mabeyo katika maisha yake ya kustaafu hapo mwishoni.mwa mwezi Juni, 2022 baada ya kulitumikia Jeshi kwa muda mrefu na kwa utiifu.

Awali Jenerali Mabeyo, akiongea mbele ya Rais amesema Jeshi la Ulinzi Tanzania litaendelea kumkumbuka Dkt. Mwunyi kwa busara na hekima wakati wa kushughulikia changamoto mbalimbali ndani ya Jeshi hilo.

Rais awapa neno watendaji serikalini
Watoto watakiwa kufichua ukatili