Afara Suleiman, Babati – Manyara.
Halmashauri ya Wilaya Babati imepokea zaidi ya Shilingi Billion 1.2 zitakazo kwenda kununua Vifaa Tiba katika Vituo vya Afya, Hospitali pamoja na Zahanati ili kuboresha Sekya ya Afya.
Hayo yamesema na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Anna Mbogo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri na kuongeza kuwa fedha hizo zimetolewa na Serikali kuu ili kuhakikisha Wananchi wanapata huduma Bora.
Wakati huo huo, Naibu Waziri Nishati, Judith Kapinga ameeleza kuwa Mkoa wa Rukwa utaunganishwa na Gridi ya Taifa kupitia njia ya umeme ya msongo wa kilovoti 400 kutokea Iringa hadi Sumbawanga kupitia Mbeya na Tunduma katika Mradi wa TAZA.
Kapinga ameyasema hayo hii leo Oktoba 3, 2023 Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Josephati Kandege kwa niaba ya Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko.