Ligi kuu ya soka nchini England msimu wa 2018/19 inatarajiwa kuanza mwishoni mwa juma hili, kwa kushirikisha timu 20 zinazotoka katika majiji tofauti ya nchi hiyo.

Ligi hiyo ambayo ina mvuto duniani, itanza Agosti 10 huku Man City wakiwa mabingwa watetezi, na wanatazamia kuwa na upinzani mkubwa kutoka kwenye klabu nyingine 19 zitakazoshiriki, kwa lengo la kuwapokonya ubingwa huo.

Ligi hii ilianzishwa rasmi mwaka 1946 baada ya vita vya pili vya dunia, na msimu wake wa kwanza ulikua 1946-47, baada ya soka la ushindani kuanzishwa nchini England msimu wa 1888-89.

Kuanzia msimu wa 1946-47, ligi hii ilitambulika kama ligi darala la kwanza nchini England na Februari 20 mwaka 1992 ilibadilishwa jina na kuitwa ligi kuu ya England (FA Premier League).

Ni klabu sita pekee ndizo zimewahi kutwaa ubingwa tangu ligi hiyo ilipoanza kuitwa Ligi Kuu Ya England mwaka 1992. Klabu hizo ni Manchester United (Mara13), Chelsea (Mara 5), Arsenal (Mara 3), Manchester City (Mara 3), Blackburn Rovers (Mara 1) na Leicester City (Mara 1).

Msimu wa mwaka 2003–04, klabu ya Arsenal iliweka historia ambayo mpaka leo haijavunjwa ya kucheza michezo 38 ya ligi hiyo bila kupoteza hata mmoja.

Msimu wa 2017–18 Manchester City nao waliweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza kufikisha alama (Point) 100, baada ya kucheza michezo 38 ya ligi.

Ifuatayo ni orodha ya klabu zilizowahi kutwaa ubingwa wa ligi hiyo na washindi wa pili kuanzia msimu wa kwanza wa 1946-47.

1946-47 – Liverpool (Bingwa), Manchester United (Mshindi Wa Pili), 1947-48 – Arsenal (Bingwa), Manchester United (Mshindi Wa Pili), 1948-49 – Portsmouth (Bingwa), Manchester United (Mshindi Wa Pili), 1949-50 – Portsmouth (Bingwa), Wolverhampton Wanderers (Mshindi Wa Pili), 1950-51 – Tottenham Hotspur (Bingwa), Manchester United (Mshindi Wa Pili), 1951-52 – Manchester United (Bingwa), Tottenham Hotspur (Mshindi Wa Pili) na 1952-53 – Arsenal (Bingwa), Preston North End (Mshindi Wa Pili).

1953-54 – Wolverhampton (Bingwa), Wanderers West Bromwich Albion (Mshindi Wa Pili), 1954-55 – Chelsea (Bingwa), Wolverhampton Wanderers (Mshindi Wa Pili), 1955-56 – Manchester United (Bingwa), Blackpool (Mshindi Wa Pili), 1956-57 – Manchester United (Bingwa), Tottenham Hotspur (Mshindi Wa Pili), 1957-58 – Wolverhampton (Bingwa), Wanderers Preston North End (Mshindi Wa Pili), 1958-59 – Wolverhampton Wanderers (Bingwa), Manchester United (Mshindi Wa Pili), 1959-60 – Burnley (Bingwa), Wolverhampton Wanderers (Mshindi Wa Pili), 1960-61 – Tottenham Hotspur (Bingwa), Sheffield Wednesday (Mshindi Wa Pili) na 1961-62 – Ipswich Town (Bingwa), Burnley (Mshindi Wa Pili).

1962-63 – Everton (Bingwa), Tottenham Hotspur (Mshindi Wa Pili), 1963-64 – Liverpool (Bingwa), Manchester United (Mshindi Wa Pili), 1964-65 – Manchester (Bingwa), United Leeds United (Mshindi Wa Pili), 1965-66 – Liverpool (Bingwa), Leeds United (Mshindi Wa Pili), 1966-67 – Manchester United (Bingwa), Nottingham Forest (Mshindi Wa Pili), 1967-68 – Manchester City (Bingwa), Manchester United (Mshindi Wa Pili), 1968-69 – Leeds United (Bingwa), Liverpool (Mshindi Wa Pili), 1969-70 – Everton (Bingwa) Leeds United (Mshindi Wa Pili), 1970-71 – Arsenal (Bingwa), Leeds United (Mshindi Wa Pili), 1971-72 – Derby County (Bingwa), Leeds United (Mshindi Wa Pili), 1972-73 – Liverpool (Bingwa), Arsenal (Mshindi Wa Pili), 1973-74 – Leeds United (Bingwa), Liverpool (Mshindi Wa Pili) na 1974-75 – Derby County (Bingwa), Liverpool (Mshindi Wa Pili)

1975-76 – Liverpool (Bingwa), Queens Park Rangers (Mshindi Wa Pili), 1976-77 – Liverpool (Bingwa), Manchester City (Mshindi Wa Pili), 1977-78 – Nottingham Forest (Bingwa), Liverpool (Mshindi Wa Pili), 1978-79 – Liverpool (Bingwa), Nottingham Forest (Mshindi Wa Pili), 1979-80 – Liverpool (Bingwa), Manchester United (Mshindi Wa Pili), 1980-81 – Aston Villa (Bingwa), Ipswich Town (Mshindi Wa Pili) na 1981-82 – Liverpool (Bingwa), Ipswich Town (Mshindi Wa Pili).

1982-83 – Liverpool (Bingwa), Watford (Mshindi Wa Pili), 1983-84 – Liverpool  (Bingwa), Southampton (Mshindi Wa Pili), 1984-85 – Everton (Bingwa), Liverpool (Mshindi Wa Pili) na 1985-86 – Liverpool (Bingwa), Everton (Mshindi Wa Pili), 1986-87 – Everton (Bingwa), Liverpool (Mshindi Wa Pili), 1987-88 – Liverpool (Bingwa), Manchester United (Mshindi Wa Pili), 1988-89 – Arsenal (Bingwa), Liverpool (Mshindi Wa Pili), 1989-90 – Liverpool (Bingwa), Aston Villa (Mshindi Wa Pili), 1990-91 – Arsenal (Bingwa), Liverpool (Mshindi Wa Pili) na 1991-92 – Leeds United (Bingwa), Manchester United (Mshindi Wa Pili),

 

ILIPOANZA KUITWA LIGI KUU YA ENGLAND

1992-93 – Manchester United (Bingwa), Aston Villa (Mshindi Wa Pili), 1993-94 – Manchester United (Bingwa), Blackburn Rovers (Mshindi Wa Pili), 1994-95 – Blackburn Rovers (Bingwa), Manchester United (Mshindi Wa Pili), 1995-96 – Manchester United (Bingwa), Newcastle United (Mshindi Wa Pili), 1996-97 – Manchester United (BIngwa), Newcastle United (Mshindi Wa Pili), 1997-98 – Arsenal (BIngwa), Manchester United (Mshindi Wa Pili), 1998-99 – Manchester United (Bingwa), Arsenal (Mshindi Wa Pili), 1999-00 – Manchester United (Bingwa), Arsenal (Mshindi Wa Pili), 2000-01 – Manchester United (Bingwa), Arsenal (Mshindi Wa Pili) na 2001-02 – Arsenal(Bingwa), Liverpool (Mshindi Wa Pili).

2002-03 – Manchester United (Bingwa), Arsenal (Mshindi Wa Pili), 2003-04 – Arsenal (Bingwa) Chelsea (Mshindi Wa Pili), 2004-05 – Chelsea (Bingwa), Arsenal (Mshindi Wa Pili), 2005-06 – Chelsea (Bingwa), Manchester United (Mshindi Wa Pili), 2006-07 – Manchester United (Bingwa), Chelsea (Mshindi Wa Pili), 2007-08 – Manchester United (Bingwa), Chelsea (Mshindi Wa Pili), 2008-09 – Manchester United (Bingwa), Liverpool (Mshindi Wa Pili), 2009-10 – Chelsea (Bingwa), Manchester United (Mshindi Wa Pili), 2010-11 – Manchester United (Bingwa), Chelsea (Mshindi Wa Pili) na 2011-12 – Manchester City (Bingwa), Manchester United (Mshindi Wa Pili).

2012-13 – Manchester United (Bingwa), Manchester City (Mshindi Wa Pili), 2013-14 – Manchester City (Bingwa), Liverpool (Mshindi Wa Pili), 2014-15 – Chelsea (BIngwa), Manchester City (Mshindi Wa Pili), 2015-16 – Leicester City (Bingwa), Arsenal (Mshindi Wa Pili), 2016-17 – Chelsea (Bingwa), Tottenham Hotspur (Mshindi Wa Pili) na 2017-18 – Manchester City (Bingwa), Manchester United (Mshindi Wa Pili)

Klabu zilizowahi kutwaa ubingwa wa soka England (Kwa idadi) tangu soka la ushindani lilipoanza kuchezwa nchini  humo, kuanzia msimu wa 1888-89.

Manchester United (Mara 20), Liverpool (18),  Arsenal (13) , Everton (9), Aston Villa (7), Chelsea na  Sunderland (6), Manchester City (5), Sheffield Wednesday na Newcastle United (4), Huddersfield Town, Leeds United, Wolverhampton Wanderers, Blackburn Rovers (3), Portsmouth, Preston North End, Burnley, Tottenham Hotspur, na Derby County (2), Sheffield United, West Bromwich Albion, Nottingham Forest, Ipswich Town na  Leicester City (1).

Video: Nape, Bashe hawawezi kufukuzwa uanachama- Ridhiwani Kikwete
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 7, 2018