Nchi ya Marekani imeweka vikwazo dhidi ya mabinti wawili wa Rais wa Urusi Vladimir Putin kutokana na ukatili wa Urusi nchini Ukraine kwa kuamini kuwa mali za Putin zimefichwa na wanafamilia.

Hazina ya Marekani mnamo Jumatano, Aprili 6, iliwataja mabinti hao kuwa ni Katerina Tikhonova, mtendaji mkuu wa teknolojia ambaye kazi yake inasaidia sekta ya ulinzi ya Urusi na Maria Vorontsova, ambaye anaongoza programu za utafiti wa vinasaba zinazofadhiliwa na serikali na kusimamiwa binafsi na Putin.

Afisa mkuu wa Marekani alisema Washington inaamini kuwa mali za Putin zimefichwa na wanafamilia na Putin anaficha mabinti zake kwa kawa hakuna mengi yanayojulikana kuhusu wao kwani Ikulu ya Kremlin imeweka maisha ya familia ya Putin kuwa ya faragha bila kuonekana kwa umma.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya Urusi, Vorontsova ni mtaalamu wa endocrinologist ambaye anahusika katika kampuni kubwa ya utafiti wa matibabu inayozingatia matibabu ya saratani na mahusiano na serikali.

Vyombo vya habari vya Urusi vimemtambua Tikhonova kama mwanahisabati ambaye anaongoza msingi wa sayansi na teknolojia unaohusishwa na chuo kikuu kikuu cha serikali ya Urusi pia ni mtaalamu wa kucheza sarakasi ya roki na roli, ambaye ameshiriki katika mashindano ya kifahari ya kimataifa, kulingana na ripoti hizo.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari mwaka wa 2019, Rais Putin alikataa kujibu moja kwa moja swali kuhusu kuongezeka kwa biashara ya binti zake na uhusiano wao na serikali.

Putin, bila kukiri kwamba Vorontsova na Tikhonova ni binti zake, aliwataja kama “wanawake” tu.

“Ninajivunia wao. Wanaendelea kusoma na wanafanya kazi. Hawajihusishi na shughuli zozote za kibiashara na hawajihusishi na siasa. Hawajaribu kujisukuma popote,” Putin alisema.

Putin alisema hataki kutoa habari yoyote kuhusu familia yake kwa sababu ya maswala ya usalama. Hata hivyo, alifichua kuwa ana wajukuu, lakini hakusema ni wangapi.

Rais Wa Zambia anahudumu bila kulipwa Mshahara
Kocha Pablo alalamikia ratiba Ligi Kuu, ASFC