Maandamano yenye ghasia yameendelea nchini Afrika Kusini usiku kucha juu ya kufungwa jela kwa Rais wa zamani Jacob Zuma na kufanya uharibifu wa mali mbalimbali.

Aidha Duka moja kubwa huko Pietermaritzburg, katika Mkoa wa KwaZulu-Natal limechomwa moto leo Julai 12,2021 sambamba na uporaji na uharibifu wa mali ukiendelea.

Picha za jengo hilo likiteketea moto na usumbufu uliosababishwa na maandamano hayo zimesambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii:

Maduka makubwa Pietermaritzburg yakiungua moto baada ya maandamano hayo kushika kasi katika Mkoa wa Kwa zul Natal

Watu kadhaa wamekamatwa na barabara zimefungwa wakati vikosi vya usalama vikishughulikia vurugu zinazoendelea.

Hata hivyo maandamano hayo yanaendelea huku mahakama ya kikatiba ikisikiza rufaa ya Zuma dhidi ya kifungo chake kwa kukaidi agizo la mahakama.

Korti inafanya tathmini ya uamuzi wake wa hapo awali na huenda ikatoa maagizo baadaye ikiwa hukumu hiyo itatekelezwa.

Hersi: Tumepokea ofa kibao
Serikali yatangaza 'lockdown' Afrika Kusini