Serikali zote Duniani ili ziweze kujiendesha na kujiletea maendeleo huandaa bajeti za fedha ambazo hutumiwa kwa matumizi mbalimbali ya kimaendeleo kwa kila mwaka wa fedha na bajeti hii huidhinishwa na bunge ambalo limepewa mamlaka ya kupitisha mapato yote na matumizi ya fedha hiyo kwa serikali.

Tanzania ni moja ya nchi ambayo masikio na macho ya watanzania wote yameelekezwa kusikia kuhusu bajeti kuu ya nchi ambayo inatarajiwa kusomwa Leo Juni 14, 2022, hii ni baada ya bajeti za wizara zote kusomwa na kupitishwa na wabunge kwa ajili ya matumizi ya mwaka ujao wa fedha wa 2022/2023.

Makadirio ya Bajeti ya mwaka mpya wa fedha ya 2022/2023 inatarajiwa kuwa tirioni 41 tofauti na bajeti ya mwaka 2021/2022 ambayo ilikuwa tirioni 37.9 ambapo ongezeko ni tirioni 8.1.

Bajeti kuu ya serikali inatarajiwa kusomwa na Waziri mwenye dhamana ya Fedha Mwigulu Lameck Nchemba ambapo bajeti hiyo kuu imeainisha vipaumbele kadhaa kama kugharamia miradi yote mikubwa ya maendeleo ikiwemo Ujenzi wa bwawa la Umeme, Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Standard Geurge, Ujenzi wa bomba la mafuta Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanga.

Bajeti hii pia imeweka kipaumbele katika utoaji wa ajira mpya kwa watanzania ili kupunguza wimbi kubwa la ukosefu wa ajira ambalo limekuwa ni kilio kikubwa kwa vijana waliohitimu vyuo na kuwa mitaani.

Pia bajeti imeangalia upandishwaji wa mishahara kwa watumishi wa Umma na Upandaji wa madaraja kwa watumishi.

Bajeti pia imetengwa kwa ajili ya Zoezi kubwa la kitaifa la sensa ambalo linatarajiwa kufanyika mwaka huu Agosti 23.

Bajeti itasaidia kutekelezwa kwa mikakati mbalimbali ya serikali ya kimaendeleo kwa mwaka ujao wa fedha kwenye sekta zote za kiuchumi kama vile Afya, Elimu, Kilimo, Uvuvi, Miundombinu ya Barabara, Ulinzi na Usalama, Uwekezaji, Ardhi, mawasiliano, ustawi wa jamii, Utalii, michezo, Maji, Nishati, Madini, Ujenzi na Viwanda .

Bajeti ya tirioni 41.9 inatokana na vyanzo kadhaa vya mapato kama ifuatavyo kiasi cha 20% ya bajeti itatokana na mikopo ya Ndani, 10% kutokana na misaada na mashirika ya kimaendeleo, 2% ikitokana na fedha za ndani za halmashauri huku bajeti kuu kutokana vyanzo vya ndani vya mapato huku takribani 69% ambayo ni sawa na trilioni 28.6 ya bajeti hii itatokana na pesa za makusanyo ya ndani ya nchi.

Usomwaji wa bajeti huu kuu utaonesha sura na Dira ya muelekeo wa mwaka mpya wa fedha kwa mwaka 2022/2023 ambao utaanza Julai mosi huku waziri atakapoiwasilisha bajeti hii itaonesha vyanzo vyote vya mapato na sheria mbalimbali za fedha zitasomwa ili kuianisha misamaha ya kodi na kuwapunguzia gharama ya nafuu ya maisha wananchi kutokana na bei za baadhi ya bidhaa kupewa misamaha ya kodi na kupunguziwa kodi hasa bidhaa zinazozalishwa nchini ili kukuza viwanda vya ndani kwetu na kupunguza ushindani wa kibiashara na bidhaa zinazozalishwa nje ya nchi.

Bajeti ya Serikali kuimarisha miradi ya kimkakati
Uingereza kusafirisha wakimbizi kwenda Rwanda