Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemtaka rais wa Urusi Vladimir Putin kutoa ufafanuzi haraka juu ya jaribio la mauaji dhidi ya mwanasiasa wa upinzani Alexei Navalny.
Baada ya uchunguzi uliofanywa na Ufaransa kuthibitisha matumizi ya kemikali ya Novichok.Ikulu ya rais wa Ufaransa Elysee, imesema katika taarifa kuwa Macron alimwambia Putin kwa njia ya simu kwamba ni muhimu aeleze anayoyajua bila kuchelewa kuhusu tukio hilo la jaribio la mauaji ya mwanasiasa huyo wa upinzani.
Macron pia alimfahamisha Putin kuwa uchunguzi wao umethibitisha kama ule uliofanywa na Ujerumani kuwa Navalny alipewa sumu aina ya Novichok, hatua ambayo ni kinyume na kanuni za kimataifa za kutumia silaha za kemikali.
Kauli hii uenda inaliweka taifa la Urusi kwenye mkwamo wa kidiplomasia na mataifa ya ulaya ambayo ni moja ya soko kuu la nishati ya gesi toka Urusi.