Wakati Mahakama nchini Kenya imezuia kwa muda madaktari kutoka nje kwenda nchini humo kufanya kazi, zaidi ya madaktari 470 wameomba kazi hizo kupitia Wizara ya Afya hapa nchini.
Serikali ya Tanzania imesema kuwa mchakato wa kupokea maombi hayo pia utaendelea kwa kuwa haijapokea taarifa yoyote kuhusu zuio kutoka nchini Kenya.
Aidha, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema bado wanasubiri taarifa rasmi kutoka kwa Serikali ya nchi hiyo.
“Tunasubiri taarifa rasmi kutoka Serikali ya Kenya kwa kuwa wao ndiyo walioleta maombi kwetu. Kama kuna mabadiliko yoyote, naamini watatufahamisha rasmi,” amesema Waziri Ummy .
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa madaktari 470 wametuma maombi kati ya nafasi 500 zilizotangazwa za kwenda kufanya kazi nchini humo.
Hata hivyo, kwa upande wake msemaji wa Wizara hiyo, Nsanchiris Mwamaja amesema kuwa wamepokea maombi mengi na kusema kuwa muda si mrefu wataanza kuyapitia maombi hayo na kuanza mipango ya namna ya kufikia mipango ya kazi.

Magazeti ya Tanzania leo Aprili 2, 2017
Shule kumi zilizofanya vizuri Wilaya ya Kishapu zapongezwa