Boniface Gideon – TANGA.

Madaktari Bingwa kutoka Nchini Ujerumani, wanatarajiwa kuwasili Mkoani Tanga Julai 13 mwaka huu kwa ajili ya kutoa huduma za Kibingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga –Bombo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Tanga, Mratibu wa Kambi ya Upasuaji wa Kurekebisha Maumbile (Plastic Surgery), kwenye Hospitali hiyo Dkt. Wallace Karata alisema wageni hao watakuwepo hadi Julai 28, 2023.

Amesema, Madaktari hao wanakuja kutoa huduma kwa watanzania ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu lakini pia kwa fani yao ya upasuaji na kurekebisha maumbile ambayo haipatikani vya kutosha nchini na watatoa bure kama msaada kwa watanzania.

Mratibu wa Kambi ya Upasuaji wa Kurekebisha Maumbile (Plastic Surgery), kwenye Hospitali hiyo Dkt. Wallace Karata.

Alisema hadi sasa wagonjwa 200 wamekwisha kujiandikisha na wakiwa tayari kwa ajili ya kusubiri huduma na Julai 10, 2023 ilikuwa ni mwisho kujiandikisha na wageni hao watakapoingia Julai 14 watafanya uchunguzi wa awali na kuweza kupanga ratiba za upasuaji.

Aidha, Dkt, Karata alisema operesheni zitaanza Julai 17 hadi Julai 28, 2023 kabla ya wageni hawajaondoka nchini, huku akiwataka waliojiandikisha kutosahaua tarehe waliozopewa, ili kuepukana na usumbufu wa kupanga ratiba zao.

Hans Pluijm: Maandalizi ya kuivaa Simba yameanza
Umasikini Vijijini watia doa ukuaji wa uchumi Tanzania