Madaktari wa Upasuaji Hospitali ya Taifa ya Kenyatta wasimamishwa kazi kwa kufanya upasuaji wa kichwa kwa Mgonjwa asiyestahili.

Taarifa kutoka mkurugenzi mkuu wa hospitali hiyo, Lily Tare, zinabainisha kuwa wagonjwa wawili waliokuwa hawajitambui na mmoja kati yao ndiye alihitaji upasuaji wa kichwa ili kuondoa damu ilionekana imeviria.

Madaktari hao walibaini kosa hilo saa chache wakiwa tayari wamekwisha pasua kichwa cha Mgonjwa huyo na kubaini hana tatizo walilotakiwa kulitibu.

Lakini pia mkurugenzi huyo ameomba radhi na kusema “tunafurahi kuwatangazia umma kwamba mgonjwa huyo sasa ametibiwa na anaenedelea vizuri”

Wafanyakazi wanaochunguzwa katika sakata hilo ni pamoja na daktari wa upusuaji wa ubongo, muuguzi, mtalaam wa dawa za usingizi.

Wakenya wameeleza hisia zao katika mitandao ya kijamii ya Twitter.

 

“Ukienda na kitambi kwenye hospitali ya taifa ya Kenyatta, unaweza ukute unapelekwa wadi ya wajawazito”

 

ASFC: Young Africans yapelekwa Singida, Azam FC yabaki D'salaam
Chin Bees kuzindua album yake leo, kutoa nakala bure kwa mashabiki