Vyanzo kadhaa rasmi, pamoja na Wizara ya Mambo ya nje ya Cuba, vimethibitisha kuachiliwa kwa madaktari wawili wa Cuba, Assel Herrera na Landy Rodriguez ambao walitumwa Mandera, kaskazini mwa Kenya, karibu na mpaka wa Somalia mwaka 2018.

Mwezi Aprili 2019, wakati wakiwa njiani kuelekea kazini, madaktari hao walitekwa nyara na wanamgambo wa kundi la Al Shabab kutoka Somalia na mlinzi wao aliuawa wakati wa utekaji nyara.

Madaktari hao wawili walikuwa sehemu ya kundi la wataalamu 100 wa afya wa Cuba waliotumwa nchini Kenya Juni 2018 baada ya makubaliano ya afya yaliyosainiwa kati ya Nairobi na Havana.

Miongoni mwa madaktari waliokuwa kwenye kundi hilo kutoka Cuba ni wataalamu watano wa figo, wataalamu wa X-ray, wataalamu wa mifupa na maungio na wataalamu wa mfumo wa neva.

Wataalamu hao wamekuwa wakitoa huduma na kushauriana na madaktari wengine katika maeneo tofauti nchini Kenya.

Mshukiwa wa mauaji ya George Floyd aachiliwa kwa dhamana.
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 8, 2020