Madaktari nchini Uhispania wamebainisha kuwa wamegundua tiba ya virusi vya ukimwi vinavyoishi ndani ya damu za watu zaidi ya milioni 34 duniani.

Madaktari hao wa kitengo cha Taifa cha Upandikizaji (ONT) wameeleza kuwa walifanikiwa kutoa tiba kwa mgonjwa wa ukimwi kwa kutumia kitovu cha mwana cha mtu mwenye vina saba ambavyo havipokei Virusi Vya Ukimwi.

Madaktarihao walieleza kuwa walichukua damu ya vitovu vya watu kadhaa wenye vina saba ambavyo havipokei virusi vya Ukimwi na kuipandikiza kwa mtu mwenye virusi vya ukimwi na baada ya miezi mitatu mtu huyo alipimwa na kubainika kuwa hana tena virusi vya ukimwi.

Akizungumzia taarifa hizo, daktari wa program ya upandikizaji kutoka taasisi ya tiba ya Catalan jijini Barcelona, Rafael Duarte alimtaja mtu aliyetibiwa ukimwi kwa njia hiyo kuwa ni Timothy Brown mwenye umri wa miaka 37 ambaye alikuwa anaishi na Virusi vya Ukimwi tangu mwaka 2009. Alisema kuwa madaktari walithibitisha kuwa alipona ugonjwa huo.

Dakrtari huyo alieleza kuwa tiba hiyo iliwahi kutolewa kwa mtu mwingine na kuzaa matunda. Mgonjwa huyo alipona Virusi Vya Ukimwi lakini alikufa kwa ugonjwa wa saratani ya damu baada ya miaka mitatu.

Hata hivyo, Kaimu Mkurugenzi wa mwitikio wa taifa wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Dk. Morris Lekule alisema kuwa utafiti huo ni lazima upitia taratibu zote za kiutafiti wa afya na kuthibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kabla ya kutangazwa kuwa ni tiba sahihi ya Ukimwi.

Florentino Perez Aanika Sababbu Za Kumtimua Benitez
Utayapenda Majibu ya Mugabe kwa Mgombea urais wa Marekani aliyedai atamkamata na kumfunga jela