Wizara ya mambo ya nje imeeleza kundi la kwanza la Watanzania waliohitimu Udaktari nchini Cuba wanasafari leo Agosti 22 na kurejea nchini Tanzania  kwa usafiri wa ndege  baada ya kukwama Cuba kwasababu ya Corona.

Aidha imesema kuwa kundi hilo la watanzania  litasafiri kwa ndege maalum ya Ufaransa hadi Paris, kisha kupanda  ndege ya shirika la ndege ya Ethiopia Airline hadi Dar es salaam.

Ambapo kundi la pili la watanzania waliokwama nchini Cuba litarejea nchini tarehe 4 Septemba 2020.

Kongamano la kitaifa kuwakutanisha viongozi mbalimbali
Hakuna upungufu wa chanjo -Dkt Subi