Familia moja huko Ulaya, Georgia Kitongoji cha Clayton, imelipwa zaidi ya Tsh. Bilion 70 sawa na dola 31 za kimarekani baada ya hospitali ya Rivadales cycle pedriatics kumuumiza mtoto wao wa siku 18 wakati wakimtahiri.
Mwaka 2013 mama mmoja anayejulikana kwa jina la Stacey Wills alimpeleka mtoto wake wa siku 18 hospitalini kwa ajili ya kutairiwa ambapo madaktari walikosea na kumuumiza lakini badala ya kumpeleka chumba cha dharula walimruhusu aende nyumbani huku damu ikiwa inatoka.
Alikuwa na majeraha makubwa kiasi ambacho ilikuwa ngumu kwake kupata haja ndogo.
Mtoto huyo ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 5 alifanyiwa upasuaji mwingine ambao ulimsaidia kuweza kupata haja ndogo kwa urahisi.
Aidha madaktari wameshauri kuwa mtoto akisha balehe afanyiwe upasuaji mwingine ili kumaliza tatizo hilo kwani bila kufanya hivyo kuna uwezekano mkubwa wa mtoto huyo akifikia utu uzima kushindwa kupata mtoto.
Kabla ya kiasi hiko cha pesa kulipwa familia hiyo ilikuwa inataka kulipwa dola 100 Milioni kwa kile alichodai wakili wao kuwa madaktari hao wamesababisha mtoto huyo akija kuwa mkubwa kushindwa kupata mwenza.
Lakini baada ya kusikiliza shtaka hilo mahakama iliamuru familia hiyo ilipwe dola 31 milioni sawa na bilioni 70.