Aliyekuwa Kocha wa Klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson amefanyiwa upasuaji wa dharula wa ubongo ili kuondoa damu iliyovujia, ambapo mara baada ya upasuaji huo uliofanywa na jopo la madaktari wamesema upasuaji umefanikiwa kwa sailimia kubwa na sasa anahitaji muda wa kupumzika.
Manchester United kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter umetoa taarifa ya kuumwa kwa Sir Ferguson kwa kusema kuwa
“Tayari ameingia kufanyiwa upasuaji wa Ubongo wake na zoezi linaendelea vizuri lakini anahitaji kuwa katika Uangalizi maalum kwa msaada ili arudi katika hali yake ya kawaida”.
Kabla ya kuumwa, Sir Alex Ferguson alionekana katika mchezo kati ya Man United dhidi ya Arsenal, Old Trafford wakati wakumuaga Kocha wa Washika Mitutu wa London (Gunners), Arsene Wenger anayeondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.
Sir Alex Furguson amewahi kushinda mataji 13 ya Ligi Kuu Soka nchini Uingereza katika kipindi cha miaka 26 alipokuwa akiifundisha Manchester United kabla yakustaafu mwaka 2013.