Mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha uharibifu mkubwa wa miundo mbinu ikwemo kubomoka kwa barabara na kusombwa kwa baadhi ya madaraja hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi.

Moja ya madaraja yaliyosombwa na maji ni pamoja na daraja la Kiluvya ambalo limesababishwa usumbuifu mkubwa kwa wasafiri wanaotoka mikoani kuelekea jijini Dar es salaam hivyo kuwalazimu madereva wanapofika Chalinze kupita njia ya Bagamoyo.

Mengine ni pamoja daraja lililopo Kawe na Mbezi  jijini Dar es salaam hali ambayo imesababisha madhara makubwa kwa watumiaji wa barabara hizo ambazo ni mhimu katika shughuli za kijamii na kiuchumi.

Hata hivyo, mvua hizo ambazo zimenyesha kwa mfululizo zimesababisha mafuriko katika baadhi ya mitaa jijini humo, hivyo misaada ya haraka na ya kijamii inahitajika kwaajili ya kuwasaidia waliokumbwa na kadhia hiyo

Wawili wajeruhiwa baada ya Ndege waliyopanda kuanguka
UDART yasitisha kutoa huduma za usafiri jijini Dar