Msanii wa bongo fleva Madee ameamua kufuta video zake zote kwenye mtandao wake wa Youtube  alizowahi kufanya nchini Afrika ya kusini pia kuzuia zisipigwe kwenye kituo chochote cha habari kufuatia sakata la mauaji ya wageni  nchini humo.

Madee ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa instagram amesema kuwa hatotumbuiza nyimbo hizo kwenye onesho lake lolote kuanzia leo

Moja ya nyimbo alizofuta msanii huyo na kupiga marufuku zisipigwe kwenye runinga ni ‘Vuvula’ aliyoifanya nchini Afrika ya kusini huku ikiwa inaonesha mandhari ya nchi hiyo.

Amesema kuwa ”Binafsi wakati natoka Manzese kwenda kushoot SA plan ilikuwa ni kutangaza vivutio vya Afrika kwa ujumla kwa kuwa imani inaniambia sisi waafrika ni wamoja.

Nimefikia hatua hiyo kwa sababu ya kile wanachowafanyia waafrika wenzetu kutoka katika mataifa mengine ya Afrika.

Najua historia yake ya kupambania mtu mweusi ni miongoni mwa watu waliokuwa wakipinga utawala wa watu weupe alikuwa anapambana kuhakikisha  waafrika tunajikomboa’ ameandika Madee.

 

Video: Kijana anayepumulia mashine nyumbani kuwekewa umeme bure
Fid Q asusia tamasha la Afrika Kusini