Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishina Msaidizi wa Polis, ACP Alex Mkama ametoa elimu kwa Madereva wa maroli juu ya matumizi salama ya barabara, ili kuepusha ajali zisizo na ulazima na ambazo zinaweza kuepukika iwapo kila mmoja atawajibika.

Kamanda Mkama ametoa elimu hiyo huku akidai kumekuwa na matumizi mabaya ya barabara, ikiwemo uegeshaji wa magari barabarani, kuyatelekeza magari yaliyoharibika barabara kuu, matengenezo makubwa na madogo kwenye barabara pamoja na kulisha wanyama kando ya barabara.

Amesema, vitendo hivyo huhatarisha maisha ya watumiaji wa barabara hizo huku akitoa onyo kwa madereva ambao watakiuka agizo hilo, kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao, ikiwemo kufungiwa leseni, kulipa faini na kufikishwa Mahakamani.

Hata hivyo, Kamanda Mkama amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro bado linaendelea oparesheni maalum ili kudhibiti wizi wa mizigo katika magari hayo maarufu kama shushashusha na kuwataka madereva kutoa ushirikiano, ili kukomesha wizi huo.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 21, 2023
Wakulima, Wafugaji msigombane - ASP Mabembere