Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limezindua operesheni itayojulikana kama Nyakua Nyakua ambapo madereva wote wanaovunja sheria hawataandikiwa kulipia faini bali watanyakuliwa na kusweka mahabusu na kufikishwa mahakamani.
Hayo yameelezwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani nchini, Fortunatus Musiliimu amesema madereva watakaokutwa na makosa kama kuzidisha mwendo watafikishwa mahakamani hii ni maalumu kwa kuhakikisha madereva wanafuata sheria za barabarani kwani ameona kuwa faini wanazodaiwa wanauwezo wa kuzitoa ndio maana wanavunja sheria za barabarani.
“Tumegundua kuwa hii faini wana uwezo wa kuilipa ndiyo maana wanafanya makosa kwa kuamini kuwa watalipa sasa hakuna kuwaandikia faini tena, Dereva akizidisha mwendo (trafiki) wamnyakue, weka ndani, peleka mahakamani”. Amesema kamanda Musiliimu.
-
Video: Sugu afichua mwanaCCM aliyemtembelea gerezani, Nyumba ya waziri yauzwa kwa mnada
-
Mkuu wa Jeshi la Polisi awaamuru wananchi kuwapiga mawe Polisi
Ameongezea kuwa madereva wengi wamekuwa wakitii sheria nyakati za mchana, lakini inapofika usiku wamekuwa wakiendesha magari yao kasi na kusababisha ajali.
“Ninazunguka mikoani na ujumbe kwa madereva ni kwamba kikosi cha usalama barabarani hakijalala, iwe usiku au mchana yeyote atakayevunja sheria hatua zitachukuliwa, jana (juzi) nilikuwa Pwani nimewaeleza hivyo madereva.”
Amesema operesheni hiyo inaanza kufanyika katika mikoa ambayo inaongeza kwa ajali na tayari ameanza na
Alisema makosa yote ambayo ni vyanzo vya ajali za barabarani hayatakuwa na faini kama ilivyokuwa awali.
“Nimeshakwenda Morogoro, Iringa, Manyoni, Igunga, Singida, Tabora, Pwani na sasa naelekea Tanga na baadaye Kilimanjaro na Arusha, tunaangalia ile mikoa yenye ajali sana ndipo tunatoa maelekezo.”
Kamanda Musilimu alisisitiza kuwa kuanzia sasa madereva wasiofuata sheria za usalama barabarani watanyakuliwa kama mwewe anavyonyakua kifaranga lengo ikiwa ni kudhibiti ajali.