Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani Wilbroad Mutafungwa amewataka madereva ambao wanafanya migomo na kuacgha magari barabarani waache kitendo hicho mara moja kwani hatua kali za kisheria zitacjhukuliwa dhidi yao.
Kamanda Mutafungwa ameyasema hayo akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za makao makuu ya kikosi cha usalama barabarani jijini Dar es salaam.
Amesema Kutokana na Suala ambalo linaendelea katika mijadala na serikali juu ya mikataba na mishahara ya madereva, wapoa ambao wamekosa uvumilivu na kuamua kufanya maandamano na migomo sehemu tofauti nchini.
“Jeshi la polisi Kikosi cha usalama barabarani tunatambua kwamba madereva wana haki ya kusafiri kutoka eneo moja kwenda eneo jingine, lkini pia abitai wana haki ya kusafirishwa na mizigo yao, hivyo tunapinga kitendo cha baadhi ya watu kuwashawishi baadhi ya madereva kufanya migomo ya aina mbalimbali. Wanatakiw akujua kwamba hali hiyo ni kosa kisheria na wajue kuna jambo wanalitafuta na kitu wanachokitafuta tutawakamata na kuwachukulia hatua,” amesema kamanda Mutafungwa.
Kamanda Mutafungwa amewataka wahusika wote wa usafirishaji kuhakikisha wanafuata taratibu na sheria za barabarani na kuhakikisha kila safari inakua salama.