Huduma ya Usafiri wa Bajaji mjini Njombe imesimama kwa takriban masaa manne kwa madai ya kushindwa kuelewa utaratibu uliokuwa ukitumika na jeshi la polisi wakati wa utekelezaji wa sheria na kufuata utaratibu kwa madereva hao, na kupelekea madereva wa daladala kuwa na mgomo siku kadhaa zilizopita.

Wakiongea kwa nyakati tofauti mjini humo madereva hao wameeleza kuwa vurugu zimesababishwa na baadhi ya madereva wenzao kushindwa kufuata utaratibu waliowekewa huku wengine wakishinikiza kufanya mgomo wa kutoa huduma hiyo.

Karimu Suleiman Ngonyani ni dereva Bajaji, anasema Mamlaka ya udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), iliwapangia utaratibu wa namna gani watakuwa wakifanya safari zao za kila siku.

Ameeleza kuwa katika kikao chao na Mkuu wa LATRA walikubaliana kufanya safari zao maeneo yote ya mji huo ambapo baada ya muda mfupi makubaliano hayo yamekwenda tofauti baada ya polisi kuanza kuwakamata kwa kigezo cha kuingilia safari.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Issa Hassan amewataka Madereva hao kuwa watulivu katika kipindi hiki wakati serikali ikishughulikia jambo lao huku wakizingatia sheria za usalama barabarani.

Aidha, Kamanda Hassan ameitaka LATRA mkoani humo kutoa leseni kwa kuzingatia mazingira rafiki kwa madereva kuweza kufanya kazi zao vizuri na kwa usalama zaidi ili kuepuka uwepo wa mwingiliano wa kimaslahi.

Rais Samia amtumbua DC Sabaya
Miaka miwili baada ya kuzikwa, mwili wa Mugabe watakiwa kufukuliwa