Baraza la Madiwani Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, limepiga kura za siri za kumuondoa Meya Juma Raibu madarakani kutokana na tuhuma mbalimbali zilizokuwa zikimkabili.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Rashid Gembe akisoma taarifa za uchunguzi ya mkoa kwa niaba ya Awali akisoma taarifa ya timu ya uchunguzi ya Mkoa, amesema Meya huyo, Juma Raibu, alikuwa akikabiliwa na tuhuma mbalimbali zilizowasilishwa na madiwani wapatao 20.

Baadhi ya tuhuma hizo ni kutumia nafasi yake vibaya, kutowaheshimu viongozi wanaohudhuria vikao na mikutano ya Halmashauri, kushiriki vitendo vya rushwa katika ujenzi holela (CBD), mienendo mibaya na ukosefu wa adabu kwa madiwani wenzake, ukosefu wa maadili na kushiriki sherehe za watu wa jinsia.

Akitangaza matokeo hayo leo, mara baada ya kura kupigwa, Mkuregenzi huyo amesema jumla ya wajumbe halali waliopiga kura ni 28 sawa na asilimia 100, ambapo kura za ndio ( za kumuondoa Meya ) zilikuwa 18 sawa na asilimia 64.3, huku kura za hapana zilikuwa 10 sawa na asilimia 35.7.

Kutokana na hali hiyo alisema kwa mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Baraza la Madiwani Mwaka 2015 kifungu cha 5.2, kanuni hiyo imetumika kumuondoa madarakani Meya huyo.

Wakizungumza kwa niaba ya Madiwani wenzao, Diwani wa Kata ya Miembeni, Mohamed Mushi na Diwani wa Kata ya Mji Mpya, Abuu Shayo, wamesema wameridhishwa na uamuzi wa baraza kutokana na mwenendo mbaya aliokuwa nao Juma Raibu.

Kwa mujibu wa kununi hizo, Naibu Meya, Stewart Nathaniel ataendelea kushikilia nafasi ya Meya hadi atakapopatikana Meya mpya.

Mwakinyo avuliwa ubingwa wa Afrika
Rais wa Ufaransa ashinda duru ya kwanza ya uchaguzi wa Urais