Magwiji wa soka mjini Madrid nchini Hispania, Real Madrid wamejinasibu kuwa tayari kukaa meza moja na viongozi wa klabu ya Man Utd, kwa ajili ya kufanya biashara ya kumsajili mlinda mlango David de Gea.

Real Madrid, wameibuka na matumaini ya kuweka hadharani mpango huo kutokana na hitaji la mlinda mlango wa kutumainiwa walilonalo kwa sasa, na hawana pengine pa kuangalia zaidi ya Old Trafford ambapo yupo mkombozi ambaye wanaamini atawasaidia katika kipindi cha msimu mpya wa ligi.

Mipango waliyojipanga nayo The Galacticos kuelekea katika kikao cha mazungumzo ya usajili wa mlinda mlango huyo, ni kutaka kutoa sehemu ya fedha na kubadilishana mchezaji ili Man Utd wakubali kumsajili kipa kutoka Costa Roca, Keylor Navas ambaye amekua na nafasi hafifu ya kukaa langoni tangu aliposajiliwa msimu uliopita.

Navas, aliwahi kuwa kwenye orodha ya wachezaji waliokua wanahitajika kwenye utawala meneja wa Man Utd, Louis van Gaal wakati alipokabidhiwa majukumu mara baada ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 ambazo zilifanyika nchini Brazil.

Hata hivyo mpango huo haujazungumzwa na viongozi wa Man Utd ambao wameonyesha kuwa kibiashara zaidi katika suala la kuuzwa kwa De Gea, ambaye aliachwa nje ya kikosi kilichopambana kwenye mchezo wa hatua ya mtoano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Club Brugge.

Rais wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez amekua katika harakati za kukamilisha mapendekezo ya meneja wa klabu hiyo Rafael Benitez ya kusajiliwa kwa baadhi ya wachezaji ambao wanahisiwa watapeleka mabadiliko ya kiuchezaji huko Estadio Stantiago Bernabeu.

Liverpool Yatangaza Vita Dhidi Ya Juventus
Bilic Alia Na FA, Adai Adrián Hakustahili Adhabu