Video na picha za tukio linalomuoenesha aliyekuwa naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai akimshambulia kwa fimbo kada wa CCM hadi kupoteza fahamu limezua mjadala mrefu katika mitandao ya kijamii na kuzua mjadala na mshangao kwa wananchi wengi.

Taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika zinaeleza kuwa tukio hilo lililotekea jana jioni wakati wagombea wakijinadi katika mkutano wa pamoja wa mchakato wa kura za maoni kumchagua mgombea mmoja atakaewakilisha chama hicho kuwania ubunge wa jimbo la Kongwa.

Inaelezwa kuwa mgombea mmoja alipanda jukwaani kwa lengo la kuwaomba kura wana CCM na kutoa tuhuma za ubadhilifu wa fedha katika jimbo hilo alizozielekeza kwa Ndugai, kitendo ambacho kilimchukiza mwanasiasa huyo.

Zamu ya Job Ndugai kuomba kura iliwadia ambapo mgombea huyo alipanda jukwaani akiwa na hasira zilizotokana na tuhuma za ubadhilifu wa fedha zilizotelewa dhidi yake. Alikanusha vikali tuhuma hizo na kuonekana mwenye hasira ya hali ya juu akinuia kumuadhibu mgombea huyo.

Ndugai alifanikiwa kumpata Ngatunga na kuanza kumshambulia kwa fimbo yake anayotembea nayo wakati wote wa mchakato huo. Naibu Spika huyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo hilo, alimshambulia Ngatunga kwa kumpiga tumboni na kichwani kabla hajapoteza fahamu.

Wakati Ndugai anampiga Ngatunga, Dkt Cholongani alionekana akimpiga picha kwa kutumia simu yake ya mkononi. Ndugai aligundua aligundua baadae na kuanza kumshambulia pia Dkt Cholongani ili asiendelee kumpiga picha.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime alipoulizwa na vyombo vya habari kuhusu tukio hilo, alisema hajapata taarifa kuhusu tukio hilo.

Vurugu katika mchakato wa kuwachuja wagombea wa CCM zinaendelea kuripotiwa katika maeneo mbalimbali nchini ambapo leo kumekuwapo na taarifa kuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Bunda, Stephen Wassira amempiga ngumi mmoja kati ya viongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya.

Lowassa kuchukua Fomu ya Kugombea Urais Kesho
Benzema Awapandisha Mzuka Mashabiki Wa Arsenal