Maelfu ya raia nchini Italia wameandamana katika mitaa mbalimbali ya mji wa Roma kupinga sera za kiuchumi za serikali ya nchi hiyo.
Waandamanaji hao wamedai kuwa serikali ya nchi hiyo iliyoingia madarakani mwaka 2018 imeshindwa kushughulikia tatizo la kukosekana kwa ajira pamoja na ubaguzi wa rangi.
Aidha, muungano wa vyama vya Wafanyakazi nchini Italia umesema kuwa kwa muda mrefu uchumi wa nchi hiyo umekua ukikua taratibu na pia hakuna ajira za kudumu hasa kwa kundi la vijana.
Hata hivyo, muungano huo umefafanua kuwa kiwango cha watu wasio na ajira nchini Italia ni asilimia 9.7 na hivyo kuifanya nchi hiyo kuwa ya tatu katika nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) baada ya Ugiriki na Hispania zenye kiwango kikubwa cha watu wasio na ajira.