Mashirika ya misaada ya kibinadamu yamesema, Somalia inakabiliwa na hali mbaya huku maelfu ya watu yakiwa yamo hatarini kutokana na tathimini iliyofanywa hivi karibuni kuhusu uhakika wa chakula na lishe.
Baa la njaa, linadaiwa kujitokeza katika wilaya za Baidoa na Burkhakaba zilizopo jimbo la Bay, huku hali ikionekana huenda itakuwa mbaya zaidi iwapo hadi Machi 2023kutakuwa hakuna msaada wa kibinadamu.
Mashirika hayo, yamesema watu mamilioni wanakabiliwa vikali vya njaa, huku wanawake hasa wajawazito, wanaonyonyesha na watoto wa chini ya umri wa miaka mitano wakiwa ni miongoni mwa walio katika hatari na wakihitaji usaidizi wa haraka.
Aidha wanasema, upo uwezekano mkubwa wa madhila kadhaa ya kusikitisha, huku wakikumbusha kuwa wakati wa njaa ya mwaka 2011, karibu zaidi ya asilimia 50 ya watu 250,000 walikufa kabla ya tamko rasmi la baa la njaa na nusu yao walikuwa ni watoto.