Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameahirisha utaratibu wake wa kila Ijumaa wa kutoa baraka kwa waumini kutokana na kuumwa mafua.
Papa anaumwa wakati ambapo kuna mripuko wa virusi vya Corona nchini Italia, yalipo makao makuu ya kanisa katoliki Vatican city, huku zaidi ya watu 650 wakiwa wameambukizwa nchini humo.
Ofisi ya Vatican imesema kuwa Papa Francis, mwenye umri wa miaka 83 aliadhimisha Ibada ya Misa kama kawaida leo asubuhi na kusalimiana na waumini mwishoni.
Alipanga kuendelea na mikutano yake binafsi kama kawaida, lakini aliamua kuahirisha kukutana na waumini.
Hata hivyo, Vatican haija thibitisha kile achomsumbua Papa Francis, lakini alikuwa na kikohozi kikali wakati wa Ibada ya Misa ya Jumatano ya Majivu, wiki hii.