Lydia Mollel, Kilosa – Morogoro.

Mtu mmoja amefariki dunia huku kaya zaidi ya nyumba 150 zikisombwa na maji katika kata ya Mvumi na Ludewa Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro, kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha katika Mikoa ya Manyara, Singida na Dodoma zilizovunja kingo za Mto wa Wami na hivyo maji kukosa elekeo na kusababisha mafuriko.

Akidhibitisha kifo hicho kilichosababishwa na maafuriko hayo, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka amesema tayari wameshafanya tathmini ya madhara yaliyosababishwa na maji hayo pamoja na kutoa msaada kwa wananchi waliokumbwa na maafa hayo.

Amesema kifo cha mtu mmoja kimesababishwa na jaribio lakutaka kuvuka maji ndipo maji yakamzidia na kumburuza hadi kupoteza maisha na pia maiti yake ilipatakina na imeshakabidhiwa kwa familia kwa ajili ya taratibu za maziko.

“Lakini pia Wananchi waliopata madhara wanaendelea kupatiwa huduma muhimu ikiwa ni pamoja na eneo la kujihifadhi kwa muda , tiba kwa wale wote waliopata changamoto za kiafya,” amesema Shaka.p

Nao baadhi ya Wananchi wa kilosa, wameshukuru jitihada mbalimbali zinazoendelea kufanyika kwa waathirika, huku wakitakiwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya mvua zinazoendelea kunyesha licha ya kuonekana kuwa sio kubwa lakini pia watambue kuwa kuna Mito mikubwa inayopokea maji kutoka sehemu Mbalimbali.

Agizo la Rais Samia laendelea kutekelezwa Katesh
Askari waliofariki kwa ajali Njombe waagwa