Vituo vya mafuta nchini leo asubuhi vimeanza kutumia bei mpya ya mafuta iliyotangazwa na serikali ikiwa na ongozeko la zaidi ya asilimia 11.82 kwa mafuta ya petrol kwa kila lita moja, asilimia 14.65 kwa mafuta ya diesel na asilimia 22.75.

Akitangaza rasmi kuanza kutumika kwa bei mpya, Mkurugenzi Mtendaji wa EWURA, Felix Ngamlagosi amesema kwa mkoa wa Dar es Salaam petrol itauzwa kwa shilingi 2,198 kwa lita, Diesel Shilingi 2,043 kwa lita na mafuta ya taa yatauzwa kwa shilingi 1,993 kwa lita. Ngamlagosi amesema kuwa ongezeko hilo la bei linatokana na mabadiliko ya bei katika soko la dunia.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mkuu huyo wa EWURA amesema kuwa mamlaka hiyo imeanza kuchukua hatua dhidi ya makampuni na wamiliki wa vituo vya mafuta waliobainika kuwa walificha nishati hiyo katika kipindi cha siku mbili zilizopita kwa lengo la kupata faida zaidi kupitia bei mpya inayoanza leo.

Amesema Mamlaka hiyo imeyatumia barua makampuni hayo kuhusu ukidhi wa sheria ili yaweze kujieleza kabla ya kuchukuliwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kunyang’anywa leseni au kulipa faini kama alivyoelezwa bungeni na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, mh. Charles Mwijage alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu taarifa za kuwepo mgomo wa kuuza mafuta na uhaba wa mafuta nchini.

Pinda: Sitaugua Moyo Jina Langu Likikatwa
Chelsea Wamsaka Mziba Pengo La Cech