Mshambuliaji wa kujitoa mhanga aliyevaa vilipuzi alijilipua katika siku ya Christmas na kuua watu kumi kwenye mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.

Kwa mujibu wa CNN, mshambuliaji huyo alijilipua karibu na ofisi za Idara ya Ulinzi ambayo iko karibu na kituo kikubwa cha polisi cha Kabul.

Msemaji Msaidizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afghan, Nasrat Rahimi amesema uchunguzi unaonesha kuwa mshambuliaji alilenga Ofisi za Idara ya Ulinzi.

Aidha, Mkurugenzi wa Hospitali ya Kabul aliiambia CNN kuwa majeruhi watano wanaendelea kupata matibabu hospitalini hapo kutokana na shambulio hilo.

Ingawa tukio hilo ni la kigaidi, hakuna kundi lolote la kigaidi ambalo limedai kuhusika.

Mashambulizi ya kigaidi jijini Kabul yakilenga Serikali na taasisi zisizo za kiserikali yameendelea kuripotiwa, ambapo mwezi uliopita watu wenye silaha walivamia kituo kimoja cha runinga. Watu hao walimuua mlinzi na kujeruhi watu wengine watano.

Magazeti ya Tanzania leo Desemba 27, 2017
Video: Maaskofu watoa maneno mazito