Watu wanne wanaosadikika kuwa ni magaidi wamekamatwa nchini Italia na Kosovo kwa tuhuma za kupanga njama na kutishia kumuua kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis.

Watu hao ambao wamebainika kuwa na uhusiano na magaidi wa kundi linalojiita Islamic States, walikamatwa na kikosi maalum cha kupambana na ugaidi nchini humo kilichokuwa kikiwafuatilia walipopanga njama hizo na kuweka vitisho kwenye mitandao ya kijamii.

Polisi nchini Italia wamesema kuwa watu hao waliweka vitisho kwenye mitandao ya kijamii na kueleza kuwa ‘Papa Francis anaweza kuwa Papa wa mwisho’.

Aidha, Papa Francis alifanya mahojiano na Carcova News na kuelezea vitisho hivyo, na hivi ndivyo alivyoeleza;

“Maisha yako mikononi kwa Mungu. Nimeshamwambia Bwana, ‘yaangalie maisha yangu’. Lakini kama ni mapenzi yako kwamba nife au kitu kingine chochote kinitokee, nakuomba kitu kimoja tu.. kwamba kisinipe maumivu. Kwa sababu mimi ni binadamu mwenye hisia kali hasa linapokuja suala la maumivu ya mwili’.”

 

Mahakama Kuu Yamtaka Kafulila Kulipa Milioni 7.5
Hitz Fm Ya Zanzibar Yachomwa Moto, Mtangazaji Asimulia Alivyonusurika Kukatwa Shingo