Mji Mkuu wa Indonesia, Jakarta umekumbwa na shambulizi la kigaidi saa chache zilizopita, huku mabomu ya kujitoa mhanga zaidi ya saba yanadaiwa kuchukua uhai wa watu saba.

Inaelezwa kuwa bomu la kwanza lilisikika majira ya saa nne na nusu asubuhi kwa saa za huko karibu na makutano ya barabara ya Thamrin na mitaa ya Wahid Haysim.

Moja kati ya mabomu yaliyolipuliwa na watu waliojitoa mhanga yanadaiwa kutokea karibu na makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika barabara ya Thamrin.

Watu takribani 14 wenye silaha, wengine wakiwa na pikipiki na wengine wakiwa na mabomu ya grinedi wamehusishwa na mashambulizi hayo.

Msemaji wa Jeshi la Polisi la nchi hiyo ameeleza kuwa watu wanne wenye silaha wanaotuhumiwa kutekeleza tukio hilo wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi.

Rais wa Indonsia, Joko Widodo amelaani mashambulizi hayo. “Taifa na watu kwa ujumla hatupaswi kuogopa na kushindwa dhidi ya mashambulizi hayo ya kigaidi,” alisema rais Widodo.

 

 

Maalim Seif amwandikia barua Papa Francis kuhusu Zanzibar, Isome hapa
Rekodi Mpya: Mtu Mzee zaidi Duniani abainika, Fahamu umri na maisha yake