Shambulizi la kigaidi la kutumia bomu lililotegwa kwenye gari limelipuka katika mgahawa mmoja maarufu ulioko ufukweni katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Kwa mujibu wa maafisa wa polisi wa Somalia, gari hilo lenye vilipuzi liligonga mgahawa wa  Lido Beach kabla ya watu watano wenye silaha kujitokeza na kuanza kurusha risasi.

Haijafahamika idadi ya watu waliojeruhiwa katika shambulizi hilo. Hakuna kundi lolote lililokiri kuhusika na tukio hilo huku vidole vikielekezwa kwa kundi la kigaidi la Al Shabaab.

Ufukwe wa Bahari, Somalia

Shambulio hilo limetokea ikiwa ni siku chache tu baada ya kundi la kigaidi la Al Shabaab kufanya shambulizi baya katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Kenya linaloendesha oparesheni maalum dhidi ya kundi hilo la kigaidi  nchini Somalia.

Wanajeshi wengi wa Jeshi la Ulinzi la Kenya waliuawa na wengine kujeruhiwa vibaya baada ya Al Shabaab kufanya shambulizi la kushtukiza katika kambi yao majira ya alfajiri wiki iliyopita.

Kundi la Al Shabaab limeeleza kuwa linawashikilia mateka baadhi ya wanajeshi wa Kenya na hivi karibuni lilitoa picha ya shambulizi hilo. Hata hivyo serikali ya Kenya haijaeleza kama picha hizo ni halisi.

 

Ushindi wa Tundu Lissu wapata baraka
Davido avunja rekodi hii kwa mamilioni ya Sony Music Global