Eva Godwin – Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa agizo, hadi kufikia Oktoba 30, 2023 Taasisi zote zenye magari yaliyoogeshwa kwa muda mrefu – TEMESA ziwe zimeyatengeneza na yaondolewe ili yaanze kazi haraka iwezekanavyo.
Akizungumza katika halfa ya kukabidhi magari na vifaa vya kazi vya ofisi za Mikoa za idara ya kazi na wakala wa usalama na afya mahali pa kazi – OSHA, hii leo Agosti 7, 2023 jijini Dodoma, Majaliwa amesema magari hutolewa ili yafanye kazi na si kuegeshwa mpaka kuharibika.
Aidha, amesema Maafisa masuhuli na Vyombo vya usalama wahakikishe wanafanya ufuatiliaji kikamilifu na kuchukua hatua kuhusu taarifa za baadhi ya madereva kujihusisha na wizi wa mafuta kwa kudanganya taarifa za umbali au kuuza mafuta kupitia vituo vya mafuta au kutoka katika magari yao.
“Vitendo hivi ni ukiukwaji wa masharti ya ajira na uhujumu kwa Serikali, hivyo tunaomba mzingatie na kufuatilia uwizi wa mafatu unaofanywa na madereva na hatua za kisheria zichukuliwe haraka iwezekanavyo,” amesema Majaliwa.
Waziri Mkuu pia amewasisitiza madereva wote wa Serikali na Taasisi zake kuzingatia sheria na taratibu za usalama barabarani na sheria za nchi akisema “nchi hii inaongozwa na Utawala wa Sheria, kuendesha gari ya Serikali haimaanishi mmepewa rungu la kuvunja sheria bali mnapaswa kuwa mfano wa kuzingatia sheria za usalama barabarani.”
Awali, Waziri wa nchi ofisi ya wazir Mkuu KAZI, Ajira, vijanaa na wenye ulemavu, Joyce Ndalichako alisema kupitia magari ambayo yametolewa leo ajira tayari 30 zimezalishwa na OSHA imepunguza tozo asilimia 15, ambazo zinaonekana ni mzigo kwa wafanyakazi.