Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limekamata magari sita yakiwa yameweka mashada ya maua kuashiria wanasafirisha msiba huku wakijua kuwa ni uongo.

Kwa mujibu wa Kamamnda wa Polisi Fortunatus Musilimu amesema manne yalitoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na mawili yalitoka Kahama yakienda Dar es Salaam.

Amesema kuwa magari hayo madogo yalikamatwa katika kizuizi cha Polisi eneo la Kingolwira Manispaa ya Morogoro, Barabara Kuu ya kuelekea Dar es Salaam.

Itakumbukwa Juni 22, 2021 watu 9 wamefariki dunia kutokana na ajali ya gari aina ya Toyota Coaster, Lori na gari dogo aina ya Toyota Cresta iliyotokea eneo la nanenane mkoani Morogoro ambapo gari hilo lilikuwa na masiba feki.

Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo afariki dunia
Mwanzilishi wa Antivirus ya McAfee afariki dunia