Shirika la Afya Duniani – WHO, linatarajia kuipatia Tanzania shilingi milioni 855 kwa ajili ya kuwezesha utafiti wa kitaifa wa viashiria vya Magonjwa yasiyoambukiza (Steps Survey 2023), unaotarajiwa kuanza mapema Agosti, 2023 nchi nzima.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo uliofanywa na Waziri wa Afya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Nassor Mazrui jijini Dodoma,Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu – NIMR, Prof. Said Abood amesema fedha hizo zitatumika Tanzania Bara na Zanzibar.

Amesema, “utafiti wa “Steps Survey” ni ufuatiliaji wa viashiria vya Magonjwa Yasiyoambukiza ili kukusanya takwimu muhimu kuhusu Magonjwa yasiyoambukiza na viashiria vya hatari vya magonjwa na itatoa taarifa muhimu na kutambua maboresho, ili kuweka mikakati ya kuboresha Matendo hayo kwa lengo la kuimarisha afya ya Jamii.”

Kwa upande wake, Mwakilishi wa WHO Dkt. Alphoncina Nanai alisema Magonjwa yasiyoambukiza yameanza kuwa tatizo kubwa ulimwenguni na katika kila vifo 10, vifo saba vinasababishwa na magonjwa yasiyoambukiza ulimwenguni na watu milioni 17 wanafariki ambapo asilimia 86 ya vifo vinatoka nchi za Afrika.

Bangala ndio basi tena Young Africans
Malisa awataka wahitimu kada za afya kuwa waaminifu